Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten amewashukuru wanachama na mashabiki wa timu hiyo kwa michango wanayoendelea kutoa kwani imekuwa na msaada mkubwa kwa kikosi cha mabingwa hao wa Kihistoria wa Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Makao Makuu ya Yanga jijini Dar es salaam, Ten amewataka WanaYanga kuendelea kuchangia kadiri wanavyoweza kwani kufanya hivyo pia ni kutimiza wajibu wao.
Aidha Ten amekemea upotoshaji unaofanywa na baadhi ya vyombo vya habari ambapo anaamini vyombo hivyo vinatumika kuharibu zoezi hilo ambalo limekuwa la manufaa kwa timu.
"Hapa katikati kumeibuka na watu ambao hawaitakii mema klabu yetu, lengo lao ni kuhakikisha kwamba kile ambacho klabu inakihitaji kutoka kwa wanachama wake hakifanikiwi," alisema Ten
"Watu wote tunafahamu uwepo wa Mwenyekiti wetu, Yusuf Manji lakini mtu kwenda kuandika kuwa Manji ameleta milioni 300 kwenye timu wakati bado mwenyewe hana uhakika na hilo jambo sio sawa"

ADVERTISE HERE