FT Mlandege 0-2 Yanga

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
14 Aug 2017
FT Mlandege 0-2 Yanga
Yanga imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mlandege katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Amani visiwani Zanzibar.

Mabao ya Yanga kwenye mchezo huo ulioanza saa mbili na nusu usiku yalifungwa na Ibrahim Ajib (50) na Emanuel Martin (73).

Huu ni mchezo rasmi wa tatu wa kirafiki ambapo Yanga imeshinda michezo miwili na kupoteza mchezo mmoja.

Ilianza kwa kuichapa Singida United mabao 3-2 kisha kupoteza jana dhidi ya Ruvu Shooting.

Katika michezo hiyo rasmi, Yanga imefunga mabao matano na kufungwa matatu huku bao moja likiwa la kujifunga.

Aidha, wakati ikiwa kwenye kambi mkoani Morogoro Yanga ilicheza mchezo wa kirafiki ambao haukuwa rasmi na kuibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Moro Kids.

Kikosi cha Yanga kinaondoka kesho Jumatatu asubuhi kuelekea Pemba ambako kitaweka kambi kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, August 23.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
14h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’