Chirwa aomba arudi Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Sep 2018
Chirwa aomba arudi Jangwani
Wakati Kocha Mwinyi Zahera akiipa Yanga ramani ya ubingwa wa Ligi Kuu Bara, aliyekuwa straika wa timu hiyo, Obrey Chirwa amewatumia ujumbe mabosi wake wa zamani kuwa anataka kuvunja mkataba wake kule Misri ili tu arudi Jangwani.

Mzambia huyo amefichua kuwa anataka arejee Jangwani na kukipiga japo kwa mwaka mmoja, kwani muda mfupi tu aliotimka Yanga amejikuta akiwamisi kinoma, hivyo kuomba wamfungulie mlango mapema kipindi hiki.

Chirwa amewasilisha maombi hayo kwa njia ya sauti kwa mtandao akiwaambia Yanga wazungumze na Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Hussein Nyika ili kumpa nafasi tena na kuja kukipiga Jangwani.

Kulingana na Mwanaspoti, Chirwa amewaambia Yanga kuwa klabu yake ya sasa haijamlipa fedha za usajili na anafikiria kuvunja mkataba nao kabla mambo hayajaharibika huko Misri.

Straika huyo aliongeza, makubaliano na mabosi wa klabu hiyo juu ya malipo hayo muda umepitiliza na anaona ni bora arudi Tanzania ambako alishaizoea, pia ni jirani na kwao Zambia tofauti na Misri iliyopo Kaskazini mwa Afrika.

Aliongeza kuwa iwapo Nyika na kamati yake itakubali yuko tayari kurudi na kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo.

Aidha, Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amekiri kupata ujumbe huo lakini kasema kwa sasa hawawezi kulizungumzia kwani usajili wao kwa sasa unaanzia kwa mapendekezo ya benchi la ufundi.

β€œNimetumiwa hiyo sauti nimeisikia, tunashukuru kusikia wachezaji wengi waliondoka Yanga wanatamani kurudi hapa, ila kwa sasa hilo la Chirwa kutaka kurudi halina nafasi kwetu kwa kuwa usajili wetu siku zote umekuwa unaanzia kwa makocha na sio sisi kama viongozi,” alisema Nyika.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
10m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’