Hongera Karia na Wambura kwa ushindi TFF

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
13 Aug 2017
Hongera Karia na Wambura kwa ushindi TFF
Jana shirikisho la soka Tanzania (TFF) lilifanya uchaguzi wa kuwapata viongozi watakaoongoza shirikisho hilo kwa miaka minne.

Katika nafasi mbili za juu, yaani Rais na Makamu wake, Wallace Karia aliyekuwa Makamu wa Rais ameshinda wadhifa wa Rais wakati Michael Wambura ameibuka mshindi kwenye nafasi ya Makamu wa Rais.

Ni wazi wawili hao ushindi wao haukuwa na mashaka kwani wameshinda nafasi zao kwa ushindi wa 'kimbunga.'

Tunawapongeza kwa ushindi na sasa tunawategemea kuja na mikakati makini ili kuweza kulipeleka mbele soka la Tanzania.

Kwani sio siri Rais aliyepita Jamal Malinzi ambaye anakabiliwa na kesi Mahakamani hakuipa Tanzania mafanikio yoyote ya maana kwenye medani ya Kimataifa.

Watanzania tumechoka kuwa 'kichwa cha mwendawazimu' tunataka kuona soka letu linasonga mbele.

Wakati huu tunatarajia kuona TFF iliyo makini na sio inayounda kamati zake za kufanya maamuzi kidhabiki.

TFF ambayo haitapindisha sheria zake kuzipendelea timu fulani pale inapoonekana zimekiuka kanuni za soka.

Tunataka TFF ambayo itakuwa na msimamo sio kuyumbishwa na timu kongwe za Simba na Yanga.

Nimemsikia Karia baada ya kushinda akisema atakuwa mkali na kutotaka utani katika uongozi wake ambapo amesisitiza umakini na watendaji wake kufuata mipango ambayo watakuwa wakiipanga kwa faida ya soka la nchi ya Tanzania.

Amesema kuanzia sasa hataki ubabaishaji kwenye soka, ameeleza kuwa anataka watu ambao wapo makini kwenye kazi, hao ndiyo ambao atafanya nao kazi.

Tunamtakia kila la kheri.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’