Kikosi cha Yanga kimeondoka leo Alfajiri kwenda nchini Rwanda tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Rayon Sports kesho.
Yanga imekwenda Rwanda bila mlinzi wake wa kulia, nahodha msaidizi Juma Abdul ambaye ni majeruhi.
Yanga inakabiliwa na changamoto kujaza nafasi hiyo hasa ikizingatiwa haikufanikiwa kusajili mbadala wa Hassani Kessy aliyetimkia Nkana FC ya Zambia.
Katika mchezo huo Yanga pia itawakosa Haji Mwinyi, Papi Tshishimbi (wagonjwa), Juma Mahadhi (majeruhi), Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko (tatizo la hati za kusafiria).
Kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi mapema mwaka huu visiwani Zanzibar, katika baadhi ya michezo Yanga ilimtumia kiraka Pato Ngonyani katika nafasi ya ulinzi wa kulia.
Huenda Pato akatumika kwenye nafasi hiyo kesho.
Lakini pia beki Andrew Vicent ana uzoefu wa kucheza beki ya kulia, nafasi ambayo aliitumikia sana wakati akiichezea Mtibwa Sugar misimu mitatu iliyopita.
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amekiri kuwa na changamoto ya kuamua amtumie nani kwenye nafasi hiyo lakini amesema Yanga ina wachezaji wengi ambao wanaweza kucheza namba mbili katika mazingira ya udharura kama sasa.
Hakuna shaka Yanga itatumia dirisha dogo la usajili mwezi Novemba kusajili beki wa kulia huku Zahera akiwa pia amependekeza usajili wa mshambuliaji mwingine wa Kimataifa.

ADVERTISE HERE