Yanga kuifuata Rayon Sports usiku wa manane

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Aug 2018
Yanga kuifuata Rayon Sports usiku wa manane
Kikosi cha Yanga kinaondoka usiku wa kuamkia kesho Jumanne (saa 8:30 usiku) kuelekea Rwanda, kwa ajili ya mchezo wao wa kukamilisha hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports.

Yanga itakwenda Rwanda bila ya nyota wake Said Juma (amefiwa) huku Juma Mahadhi pamoja na nahodha wake msaidizi, Juma Abdul wakiwa ni majeruhi.

Yanga inaondoka na kikosi cha wachezaji 20 tayari kwa mchezo huo utakaochezwa Jumatano jijini Kigali.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema Abdul atakosekana kwenye mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

"Mahadhi inafahamika aliumia kwenye mchezo dhidi ya Waarabu na atakuwa nje kwa zaidi ya wiki moja sasa, lakini hata kama angekuwa mzima asingekuwapo kwenye safari kwa sababu ana kadi mbili za njano," alisema Saleh.

Alisema ukiondoa nyota hao wawili, wachezaji wengine wote wapo kwenye ari nzuri na kwamba baada ya mazoezi ya jana, kocha alitarajiwa kutangaza wachezaji watakaoondoka na timu kuwafuata Rayon Sports.

"Mpaka baadaye jioni (jioni ya jana) kocha ndipo atatangaza nani na nani wanaenda Rwanda kwa ajili ya mchezo huu wa mwisho," alisema Saleh.

Aidha, alisema licha ya kuwapo kwa safari hiyo ya Rwanda, kocha wa timu hiyo, Mwinyi Zahera, anauwazia zaidi mchezo ujao wa Ligi Kuu dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa Septemba 2, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kambarage.

"Rwanda tunaenda kukamilisha ratiba kwa sababu hatuna nafasi ya kusonga mbele, Kocha anauwazia pia mchezo wetu wa ligi ugenini dhidi ya Mwadui.

"Tunawafuata Rayon, lakini pia tunaupigia mahesabu mchezo na Mwadui," aliongeza kusema Saleh.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’