FT : Yanga 2-1 Mtibwa Sugar, Makambo habari ya mjini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Aug 2018
FT : Yanga 2-1 Mtibwa Sugar, Makambo habari ya mjini
Yanga imeanza vyema kampeni ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Tanzania Bara msimu huu baada ya kuilaza Mtibwa Sugar mabao 2-1 katika mchezo mkali uliopigwa kwenye dimba la Taifa.

Mshambuliaji Mcongoman Heritier Makambo amefungua akaunti ya mabao kwenye mchezo huo akiifungia Yanga bao la kuongoza kwenye dakika ya 31 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Gadiel Michael.



Kabla ya kufunga bao hilo, kwenye dakika ya 22 Makambo alifunga bao ambalo lilikataliwa na mshika kibendera aliyedhani alikuwa ameotea.

Hata hivyo picha za marudio ya video zinaonyesha Makambo hakuwa ameotea na Yanga ilinyimwa bao halali kabisa.



Kwanye kipindi cha kwanza Yanga ilitawala zaidi sehemu ya kiungo ikiwatumia Ibrahim Ajib aliyeingia kwenye dakika ya 14 kuchukua nafasi ya Ninja aliyeumia, Papi Tshishimbi na Feisal Salum 'Fei Toto' aliyeonyesha kiwango bora kabisa.

Yanga Ilifunga bao la pili kwenye dakika ya 41 kupitia mkwaju wa penati uliowekwa kambani na Kelvin Yondani baada ya Mrisho Ngassa kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Kipindi cha pili Yanga ilipunguza kasi na kuwapa nafasi Mtibwa Sugar kumiliki mpira kwa muda mwingi huku Yanga ikitumia mashambulizi ya kushitukiza.





Bao la kufutia machozi la Mtibwa lilifungwa na Haruna Chanongo kwenye dakika ya 73.

Mtibwa Sugar ilionyesha upinzani mkali hasa kwenye kipindi cha pili, wameonyesha kuwa moja ya timu zilizojipanga vyema msimu huu.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’