Tshishimbi kutua wakati wowote

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
13 Aug 2017
Tshishimbi kutua wakati wowote
Kiungo mkabaji aliyesajiliwa na Yanga kutoka Mbabane Swallows, Papi Kabamba Tshishimbi anatarajiwa kutua jijini Dar es salaam wakati wowote.

Taarifa za uhakika ambazo zimethibitishwa na Afisa wa Habari wa Yanga Dismas Ten ni kuwa uongozi wa Yanga uliridhia kumpa mapumziko ya siku kadhaa kiungo huyo kutokana na ushiriki wake kwenye michuano ya kombe la shirikisho hatua ya makundi.

Tshishimbi alitarajiwa kuwasili jana Jumamosi mchana kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Charles Mkwasa lakini alishindwa kujua atawasili saa ngapi baada ya kupoteza mawasiliano naye.

Mapema jana waandishi wa Habari walifurika uwanja wa ndege wa kimataifa wa julius Nyerere kumsubiri kiungo huyo

Mbabane Swallows ilitinga hatua ya makundi michuano kombe la shirikisho barani Afrika Tshishimbi akiwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa timu hiyo, alicheza michezo yote.

Yanga imekamilisha usajili wa mchezaji huyo kutoka Mbabane Swallows baada ya kuvunja mkataba wake wa miezi minne iliyokuwa imebaki na klabu hiyo ya Swaziland.

Tshishimbi alionekana na Yanga kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika wakati Mbabane Swallows ilipokuja Tanzania kucheza na Azam FC.

Alikuwa akifuatiliwa na uongozi wa Yanga tangu wakati huo.

Umahiri wake katika nafasi ya kiungo mkabaji unatarajiwa kumaliza kabisa tatizo hilo katika klabu ya Yanga
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’