Tuko tayari kuikabili USM Alger - Saleh

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2018
Tuko tayari kuikabili USM Alger - Saleh
Wawakilishi wa Tanzania waliobakia katika mashindano ya kimataifa, Yanga wamesema kuwa wako tayari kuwavaa wapinzani wao USM Alger kutoka Algeria na sasa wanasubiri muda wa mchezo huo ufike.

Mechi hiyo ya Kundi D ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika itafanyika kesho kuanzia saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh, amesema kuwa wachezaji na benchi la ufundi wameshakamilisha maandalizi na wanaamini watapata matokeo mazuri katika mchezo huo

Saleh amesema kuwa kila mchezaji anafahamu umuhimu wa mchezo huo na wametakiwa kusahau matokeo ya mechi zilizotangulia.

"Kiukweli tunamshukuru Mungu wachezaji wako salama na mipango yetu iko vizuri, tunachosubiri ni muda wa mechi tumalize kazi yetu," Saleh amenukuliwa na gazeti la Nipashe.

Aliongeza kuwa wanatarajia kurejea jijini leo baada ya kumaliza kambi yao ya wiki mbili waliyoiweka Morogoro kujiandaa na mechi hiyo ya kimataifa pamoja na msimu mpya wa ligi.

"Tumeamua kubaki Morogoro hadi kesho (leo), hii inatokana na Uwanja wa Taifa kuwa na mashindano ya vijana na hivyo tutakosa nafasi ya kuutumia kama ambavyo tumezoea," aliongeza.

Naye beki wa timu hiyo, Juma Abdul alisema kuwa wanahitaji kushinda mechi hiyo ili wapate nguvu ya kuanza vyema msimu mpya wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

"Tunajua mechi ni ngumu lakini hakuna kisichowezekana, tumeiva na tuko tayari kupambana, tunaingia uwanjani tukiwa na nguvu tofauti na tulivyokutana nao kwao," alisema beki huyo.

Tayari kikosi cha USM Alger kiko nchini tangu juzi kwa ajili ya mchezo huo utakaochezeshwa na waamuzi kutoka Namibia.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
13h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
17h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
18h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
18h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’