Yanga yapania kushinda mechi ya kwanza CAF

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jul 2018
Yanga yapania kushinda mechi ya kwanza CAF
Kocha msaidizi wa Yanga, Noel Mwandila amesema kutokana na maandalizi waliyofanya yanatosha kuwafunga Gor Mahia na kupindua matokeo ya mechi ya kwanza.

Yanga walifungwa 4-0, Gor Mahia ya Kenya kwenye Uwanja wa Kasarani, Nairobi watarudiana kesho kwenye Uwanja wa Taifa katika mechi ya Kundi D.

Mwandila alisema kuongezeka kwa baadhi ya wachezaji ambao walikosekana katika mechi ya kwanza wataongeza nguvu katika timu hiyo.

Alisema Yanga ina kiu ya kupata ushindi wa kwanza baada ya kucheza mechi tatu bila ushindi na kushindwa kufunga hata bao.

"Kama benchi la ufundi tumejipanga na kufanya maandalizi ya kutosha ili kucheza katika kiwango kizuri tena tukiwa nyumbani na kushinda kwani hilo ndio lengo letu kuu," alisema Mwandila.

"Hatukuwa imara katika mechi za mwanzo kwani tulikuwa tukifanya makosa mengi lakini tumeyaona na kuyarekebisha hayo na jukumu limebaki kwa wachezaji, " alisema Mwandila.

Nahodha wa Yanga, Juma Abdul amesema wachezaji wenzake wote wanamorali ya hali ya juu ili kupambana na kuhakikisha wanapata ushindi.

"Kuanzia kambini mpaka mazoezi kila mchezaji yupo na hali na morali kuhakikisha tunashinda kwa mara ya kwanza tukiwa nyumbani," amesema Abdul.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’