Nsajigwa akomaa na safu ya ulinzi

Yanga Damu By Yanga Damu
β€’
8 Aug 2017
Nsajigwa akomaa na safu ya ulinzi
Leo asubuhi Yanga imeendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya kwenye dimba la Polisi Kurasini jijini Dar es salaam.

Mwalimu Lwandamina akisaidiana na Shedrack Nsajigwa waliwaongoza vijana katika program maalum.

Kikosi hicho cha Lwandamina kitakuwa na kibarua kizito cha kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Bara kuanzia Agosti 27 itakapocheza dhidi ya Lipuli kwenye Uwanja wa Taifa.

Yanga ilianza maandalizi ya msimu mpya kwa kufanya mazoezi ya Gym jijini Dar es salaam kabla ya kwenda mkoani Morogoro ambapo waliendelea na mazoezi ya kujenga utimamu wa mwili kwa kukimbia na mapalashuti.

"Tumejiandaa na tunaweza kuanza ligi, ni wazi kuwa msimu huu utakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu timu nyingi zimejiandaa na hata kusajili vizuri," amesema Lwandamina.

Katika mazoezi ya leo asubuhi kwenye Uwanja wa Polisi Kurasini, Nsajigwa alikuwa akitilia mkazo namna ya ukabaji.

Yanga inajiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba utakaofanyika Agosti 23, jambo lililomfanya Nsajingwa kuwa mkali kwa makosa ya kizembe yaliyokuwa yakifanywa na mabeki wake.

Mara zote Nsajigwa alionekana kuwa mkali kwa makosa hayo na kulazimika kukaa na mchezaji mmoja mmoja ili kutoa maelekezo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’