Baada ya ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Singida United katika mchezo wa kirafiki uliopigwa kwenye dimba la Taifa Jumamosi iliyopita, Yanga itashuka tena dimbani wikiendi ijayo kucheza mchezo wa pili wa kirafiki.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Yanga Dismas Ten, amesema mchezo huo utapigwa kati ya Jumamosi au Jumapili dhidi ya mpinzani ambaye atawekwa hadharani baadae.
Aidha kikosi cha Yanga leo kimeendelea na mazoezi jijini Dar es salaam.
Juzi akizungumzia mchezo wa kwanza wa Yanga tangu itoke Morogoro, Kocha George Lwandamina alisema kuwa wachezaji wake hawakucheza vizuri kutokana na mazoezi magumu waliyofanya kwa wiki tatu mfululizo.
Amesema wachezaji kuwa wazito baada ya kutoka kwenye mazoezi magumu ni jambo la kawaida lakini anaamini michezo kadhaa ya kirafiki itawarudisha kwenye kiwango cha chao.

ADVERTISE HERE