Abbas Tarimba ndiye aliyefanikisha walinzi Kelvin Yondani na Hassani Kessy waliokuwa karibu kabisa kutimka waendelee kubaki Jangwani.
Baada ya Mkutano uliofanyika baina yake na viongozi wa Yanga, Bosi huyo wa kampuni ya SportPesa kwa upande wa Tanzania, ndiye anayewezesha upatikanaji wa pesa wakati huu ili kukamilisha usajili.
Dirisha la usajili litafungwa Alhamisi ijayo, Julai 26 2018 na TFF tayari imetahadharisha kuwa hakutakuwa na muda wa ziada.
Yanga imekuwa na wakati mgumu sana kukamilisha michakato ya usajili wa baadhi ya wachezaji wapya pia kuhuisha mikataba iliyomalizika kutokana na 'ukata'.
Wengi walitarajia baada ya taarifa kuwa Mfanyabiashara Yusufu Manji ameridhia kurejea kwenye nafasi yake ya uwenyekiti, klabu hiyo ingepata ahueni ya kiuchumi.
Hata hivyo imeelezwa Manji ameomba apewe angalau miezi mitatu ili ajipange kabla ya kurejea rasmi jambo lililoilazimu Yanga wakati huu kusaka fedha kutoka vyanzo tofauti tofauti.

ADVERTISE HERE