Klabu ya Singida United imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo wa JKU Feisal Salum Abdalah kwa mkataba wa miaka mitatu.
Fei Toto ameng'ara kwenye mashindano ya kombe la Kagame yanayofikia tamati kesho jijini Dar es salaam.
Kiungo huyo ameonyesha uwezo wa hali ya juu na kumfanya awe miongoni mwa wachezaji bora wa michuano hiyo mwaka huu.
Singida United ilianza mchakato wa kumsajili kiungo huyo mapema hata hivyo mchakato huo ulikwama awali baada ya JKU kuweka ngumu kwa kuwa alikuwa na mkataba na timu hiyo.
Uongozi wa Singida United umesema katika kikao cha pamoja cha Uongozi wa JKU, wamekubaliana gharama za kufidia mkataba wa miaka miwili ambayo mchezaji huyo alibakiza kuitumikia JKU.
Mapema mwaka huu Yanga iliwahi kufanya mazungumzo na Fei Toto baada ya kukamilika kwa michuano ya kombe la Mapinduzi ikaelezwa walifikia makubaliano na kiungo huyo.
Hata hivyo tayari Yanga imekamilisha usajili wa kiungo mwingine kutoka Zanziba Mohammed Issa 'Banka' aliyekuwa akiichezea Mtibwa Sugar.

ADVERTISE HERE