Ujio wa Banka, Kamusoko ajipange

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
12 Jul 2018
Ujio wa Banka, Kamusoko ajipange
Mohammed Issa 'Banka' ametua Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Mtibwa Sugar, mabingwa wa kombe la FA.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema hawajakurupuka kumsajili Banka. Amesema wamekuwa wakimfuatilia kwa muda kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu.

Banka amekabidhiwa jezi namba nane ambayo msimu uliopita ilitumiwa na kinda Maka Edward. Mapema mwezi Juni Maka alitangaza kuiacha jezi hiyo kwa ajili ya 'heshima' ya mchezaji anayekuja kuitumia.

Ujio wa Banka utaimarisha safu ya kiungo ya Yanga pia huenda utamrejesha Tshishimbi kwenye namba yake ya kiungo mkabaji.

Msimu uliomalizika mapungufu katika sehemu ya kiungo yalipelekea Yanga wakati mwingine imtumie Tshishimbi kama kiungo mshambuliaji.

Ujio wake pia unamaanisha kiungo mkongwe Thabani Kamusoko itabidi ajipange kwelikweli kwani atakabiliwa na ushindani mkali wa namba kutoka kwa Banka.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
32m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
21h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’