Tarimba kufunguka zaidi kilichomuondoa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jul 2018
Tarimba kufunguka zaidi kilichomuondoa Yanga
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mpito ya kuivusha Yanga Abbas Tarimba amepanga kuzungumza na waandishi wa habari leo kubainisha yaliyopelekea kujiuzulu kwake.

Jana Tarimba alitangaza kujiuzulu nafasi yake kwa kile alichoeleza kuingiliana kwa majukumu baina ya Kamati yake na Kamati nyingine za Yanga.

Kamati ya Tarimba iliundwa Juni 10 2018 kwenye Mkutano Mkuu wa Wanachama uliofanyika bwalo la Polisi, Osterbay jijini Dar es salaam.

wanachama wa Yanga kupitia Bodi ya Wadhamini ya klabu hiyo waliunda Kamati ya watu tisa chini ya Tarimba Abbas ikiwa na lengo la kusimamia Shughuli mbalimbali za klabu hiyo kufuatia kile kinachoonekana kuelemewa kwa uongozi uliopo madarakani sasa chini ya Kaimu Mwenyekiti, Sanga.

Kamati hiyo iliwajumuisha Tarimba Abbas akiwa Mwenyekiti, Makamu wake, Saidy Mecky sadik na Wajumbe wa Kamati hiyo wakiwa Abdallah Bin Kleb (amejiuzulu), Hussein Nyika, Samuel Lukumay, Lucas Mashauri, Yusuphed Mhandeni, Hamad Islam, Makaga Yanga, Ridhiwani Kikwete, Majjid Suleiman na Hussein Ndama.

Tarimba ameutuhumu uongozi wa Yanga chini ya Kaimu Mwenyekiti Clement Sanga kuwa haukuwa tayari kushirikiana na Kamati hiyo.

Juzi kwenye Mkutano wa Wenyeviti wa Matawi ya klabu ya Yanga, Sanga alidai tangu kuundwa kwa Kamati ya Tarimba hakuna lolote walilokuwa wamefanya.

Sanga alisema Kamati ya Tarimba ilipewa jukumu moja tu, la kutafuta pesa kwa ajili ya usajili na kuhuisha mikataba ya wachezaji iliyomalizika jukumu ambalo hawajalitekeleza mpaka sasa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’