Manji bado hajajibu barua ya Yanga, uongozi wampa muda zaidi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Jul 2018
Manji bado hajajibu barua ya Yanga, uongozi wampa muda zaidi
Mkutano wa Yanga uliofanyika kwenye Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam mwezi uliopita, miongoni mwa maazimio yake ilikuwa ni wanachama hao kuazimia Yusup Manji kutengua uamuzi wake wa kujiuzulu wadhifa wake wa uenyekiti.

Uongozi wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika umeeleza kwamba kuchelewa kujibu barua ya kuombwa atengue maamuzi ya kujiuzulu wadhifa wake huenda kigogo huyo akawa na majukumu mengi yamembana.

Nyika ameeleza kuwa bado Manji kweli hajajibu barua yao na ikumbukwe katika Mkutano Mkuu wa wanachama wa klabu hiyo waliazimia kupinga kujiuzulu kwake na kupendekeza aendelee kuwa mwenyekiti wao.

Mwenyekiti huyo amefafanua kwa kusema yawezekana labda akawa ametingwa na majukumu yake binafsi kikazi.

Nyika amesema wamempa muda mpaka pale atakapopata nafasi ya kuwajibu kwa maana hivi sasa bado hakuna chochote ambacho kimewafikia kutoka kwake tangu wamtumie barua hiyo.

Kupitia Kamati ya kuipigania Yanga wakati wa Mpito, Nyika amesema inaendelea kufanya kazi ya kusaka fedha kwa ajili ya kuisaidia Yanga ili iweze kufanya usajili na kuiwezesha klabu kuhusiana na ulipaji wa mishahara ya wachezaji.

Nyika ameielezea kamati hiyo kuwa si kwamba inatoa fedha bali inafanya mipango ya kutafuta watu watakaotoa fedha ili klabu iweze kutekeleza majukumu yake ikiwemo usajili na mengine.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’