Wenyeji wa michuano ya kombe la dunia Urusi wametinga robo fainali baada ya kuwaangusha moja ya vigogo wa Ulaya, Hispania kwa mikwaju ya penati 4-3 kufuatia sare ya bao 1-1.
Mchezo huo ulipigwa kwa dakika 120 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa 1-1.
Hispania ilitangulia kufunga kwenye dakika ya 12 kwa mlinzi wa Urusi, mkongwe Ignashevic kuutumbukiza mpira katika lango lake.
Urusi iliyocheza kwa kujihami zaidi ilifanikiwa kusawazisha kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 41 baada ya Gerrard Pique kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Artem Dzyuba alifunga mkwaju huo ulioirejesha Urusi mchezoni.
Hispania ilitawala kwa karibu dakika zote lakini walishindwa kupenya ngome ya Urusi iliyokuwa na wachezaji wote 10 nyuma ya mpira.
Wakati Urusi ikifanikiwa kufunga penati zote, Iago Aspas na Koke walikosa mikwaju yao kwa upande wa Hispania.
Hakuna aliyetegemea kama Hispania itaondoshwa kwenye michuano hiyo lakini ni matokeo yaliyopokewa kwa furaha na mashabiki wa Urusi.
Urusi inasubiri mshindi kati ya Croatia dhidi ya Denmark kwa mchezo wa robo fainali.

ADVERTISE HERE