Koukpo katimka lakini Mcongo mambo safi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Jun 2018
Koukpo katimka lakini Mcongo mambo safi
Baada ya kutimka mshambuliaji raia wa Benin Marcelin Koukpo, Mcongo Heritier Makambo huenda akamwaga wino Jangwani imefahamika.

Jana Yanga iliendelea na mazoezi kwenye chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam ikiwa na makundi mawili ya wachezaji, wapya wanaofanya majaribio na wale ambao walikuwa Yanga tangu msimu uliopita.

Makambo aliyetua na Zahera wiki iliyopita amekuwa akionyesha kiwango kizuri kwenye mazoezi huku akionekana yuko 'fiti' kwa kumudu ipasavyo mazoezi anayopewa.

Makambo jana alijumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji walioitumikia Yanga msimu uliopita. Hii ni dalili kuwa mchazaji huyo tayari amefuzu majaribio.

Kuondoka kwa Koukpo kumeibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki wa Yanga lakini ukweli ni kwamba kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera hakuridhishwa na uwezo wake.

Inaelezwa Koukpo hakumvutia kabisa Zahera kwani hakuwa akimudu mazoezi aliyokuwa akitoa tofauti na wenzake waliokuwa wakijaribiwa naye.

Baada ya shinikizo la kusajiliwa kukwama, Kuokpo anadaiwa kuondoka kimyakimya bila kuaga licha ya kuwa aliahidi kuhudhuria mazoezi jana.

Taarifa zaidi zinabainisha kuwa Koukpo alikaribia kusajiliwa kabla ya Zahera kumuwekea ngumu kwani tayari alikuwa ameshafanyiwa vipimo vya afya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’