Yanga imefunga mjadala wa mlinda lango

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Jun 2018
Yanga imefunga mjadala wa mlinda lango
Jana Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga Hussein Nyika alisema timu hiyo haina mpango wa kusajili kipa mwingine na ilikuwa mbioni kuhuisha mkataba wa Benno Kakolanya.

Nyika alithibitisha kuwa Kakolanya aliyekuwa akihusishwa na JKT Tanzania bado yuko kwenye mipango ya Yanga hivyo ataendelea kubaki Jangwani.

Kakolanya mwenyewe wakati akihojiwa na Sport Leo ya Radio One, alieleza sababu iliyomfanya ashindwe kuitumikia Yanga ipasavyo msimu uliomalizika kuwa ni majeraha ya goti.

Ilikuwa ikivumishwa kuwa mlinda lango huyo mwenye umri wa miaka 23 alikuwa akigoma kucheza kushinikiza alipwe pesa za usajili.

Mwenyewe amekanusha kuwa taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote na ndio maana ameridhia kubaki Yanga.

"Mimi nilikuwa nasumbuliwa na goti msimu mzima, kama ningekuwa nagoma basi nisingekuwa nakaa hata benchi kwenye baadhi ya michezo."

Kakolanya amesema kwa sasa amepona majeraha yake na yuko tayari kuitumikia Yanga kikamilifu.

Kipa huyo alienda mbali zaidi kwa kusema hahofii ushindani wa namba dhidi ya wapinzani wake Rostand na Kabwili kwa kuwa anaamini kila mmoja ana uwezo wake tofauti ambao mwingine hana.

Yanga ilikuwa ikisaka mlinda lango hasa baada ya kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera kutorishishwa na kiwango cha Youthe Rostand ambaye bado ana mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuichezea Yanga.

Baadhi ya walinda mlango akiwemo Benedict Tinocco wa Mtibwa Sugar na Deo Munishi ambaye amesajiliwa na Simba jana, walikuwa wakihusishwa na mabingwa hao wa kihistoria Tanzania Bara.

Pia kipa mkongwe aliyemaliza mkataba klabu ya TP Mazembe, Vumi-Ley Matampi na kipa mwingine kutoka nchini Kenya walikuwa wakihusishwa na Yanga.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’