Hatukuwahi kuzungumza na Kagere, Wawa - Nyika

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
27 Jun 2018
Hatukuwahi kuzungumza na Kagere, Wawa - Nyika
Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amesema timu hiyo haikuwahi kuwa na mpango wa kuwasajili Meddy Kagere aliyesajiliwa na Simba jana akitokea Gor Mahia na Paschal Wawa ambaye anafanya majaribio katika klabu hiyo.

Nyika ameeleza kushangazwa na taarifa zinazodai wamezidiwa ujanja wa watani zao ambao wamekuwa wakiwasajili wachezaji wanaofanya nao mazungumzo.

"Ifahamike sisi hatushindani na timu yoyote kusajili. Tunachofanya ni kutafuta wachezaji wanaofaa ili tujenge timu imara," amesema Nyika.

"Hatujawahi kuwa na mazungumzo na wachezaji hao. Hizo ni taarifa tu ambazo zilikuwa zikiripotiwa na vyombo vya habari lakini hazikuwa na ukweli wowote," amesisitiza Nyika.

Akizungumzia hatma ya usajili wa klabu hiyo, Nyika amesema mchakato unaendelea vizuri na anaamini Yanga itakuwa na kikosi imara msimu ujao.

"Sisi tunaendelea na usajili bila ya kutangaza wachezaji hadi pale tutakapokamilisha zoezi zima. Ukimya wetu haumaanishi kwamba hatufanyi kitu."

"Wapenzi na wanachama wetu wawe watulivu. Wafahamu viongozi wao tuko makini na tutatoa taarifa baada ya kukamilisha kila kitu"

Yanga imeanza mazoezi jana ikiwa na idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni waliofika kufanya majaribio.

Mazoezi hayo yanaendelea leo katika uwanja wa chuo cha Polisi Kurasini jijini Dar es salaam.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
47m ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
15h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
19h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’