Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28m ago
Ni leo; Yanga inaanza kubonda na kunyonga CAFCL

SASA hakuna tena cha kusubiri! Mikiki mikiki ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) inaanza rasmi kwa Yanga leo, Jumamosi, Novemba 28, 2026, itakapowakaribisha MC Alger ya Algeria kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.

Mtanange huo wa kwanza wa Kundi B utapigwa kuanzia saa 10:00 jioni, huku Wananchi wakilenga kuanza kampeni yao ya kimataifa kwa kishindo mbele ya mashabiki wao.

Baada ya siku kadhaa za maandalizi, uchambuzi na hamasa kubwa kwa mashabiki, sasa ni wakati wa kikosi cha Kocha Mkuu Fadlu Davids kushuka dimbani kutekeleza kile kilichopangwa.

FADLU AMEJIPANGA

Kocha Mkuu wa Yanga, Fadlu Davids, tayari ameweka wazi hesabu zake za mchezo wa leo, akisisitiza kuwa kikosi chake kitacheza soka la kushambulia huku kikizingatia nidhamu ya kulinda lango lake.

Fadlu na benchi lake la ufundi wamefanya uchambuzi wa MC Alger, ikiwemo kuangalia mabadiliko ya kiufundi yaliyofanywa na wapinzani hao baada ya kuachana na kocha wao mkuu, Khaled Ben Yahia.

ZANZIBAR KUPAMBWA KIJANI NA NJANO

Hamasa kubwa iliyofanywa na uongozi wa Yanga katika siku za hivi karibuni, ikiongozwa na Meneja wa Habari na Mawasiliano, Ali Kamwe, imelenga kuhakikisha New Amaan Complex inafurika mashabiki wa Wananchi.

Viingilio vya mchezo huo ni kama ifuatavyo:

  • Jukwaa la Saa na Obit – Sh 5,000

  • Jukwaa la Urusi – Sh 10,000

  • Wings – Sh 20,000

  • VIP – Sh 30,000

Tiketi bado zinapatikana kupitia mfumo wa Lipa Tiketi kwa kupiga msimbo 14946*11# au kutembelea tovuti ya http://yanga.lipatickets.tz/.

NI SIKU YA KUBONDA NA KUNYONGA!

Yanga inahitaji kuutumia vyema uwanja wa nyumbani, kuonyesha makali yake mbele ya mabingwa wa Algeria na kutuma ujumbe kwa wapinzani wengine wa Kundi B, Club Africain ya Tunisia na Zamalek ya Misri.

Baada ya misimu miwili mfululizo ya kukwama katika hatua ya makundi, Wananchi wanataka kuandika simulizi mpya katika michuano hiyo.

Safari ya kutinga robo fainali inaanza leo, na pointi tatu dhidi ya MC Alger ndizo hesabu za kwanza.

Yanga SC Stories

Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL
Mayele anaamini huu ni mwaka wa Wananchi CAFCL
14m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
Aziz Ki awapa ujumbe mashabiki Yanga 'tutapambana'
18h ago
READ MORE β†’
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
Fadlu aichambua MC Alger, aweka mkakati wa ushindi
18h ago
READ MORE β†’
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
Wananchi wajitokeza kuchangia damu Viwanja vya Maturembeta Zanzibar
20h ago
READ MORE β†’
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
Tuko tayari kuikabili MC Alger - Job
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
Yanga yakamilisha maandalizi New Amaan Complex tayari kuikabili MC Alger
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
Aziz Ki aweka ahadi, apania ligi ya mabingwa
1d ago
READ MORE β†’
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
CAFCL msimu huu VAR kuanza kutumika hatua ya makundi
1d ago
READ MORE β†’