Uongozi wa klabu ya Yanga leo umeendesha zoezi la uchangiaji damu viwanja vya Maturembeta Zanzibar ikiwa sehemu ya matukio ya kusaidia Jamii.
Yanga iko visiwani Zanzibar ambapo kesho Jumamosi itashuka uwanja wa New Amaan Complex kuikabili MC Alger katika mchezo wa kwanza kundi B CAFCL.
Mashabiki na Wanachama wa Yanga wameendelea kujitokeza kushiriki zoezi hilo la kuchangia damu ili kuokoa maisha.


