Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24m ago
Yanga kuelekea Zanzibar leo, maandalizi ya kuikabili MC Alger

Kikosi cha Yanga leo kinaelekea visiwani Zanzibar kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa kwanza hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL) dhidi ya MC Alger.

Mtanange huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini utapigwa Jumamosi, Novemba 28 kwenye uwanja wa New Amaan Complex.

Baada ya mapumziko ya mwishoni mwa wiki, Yanga ilianza maandalizi yake jana, kikosi kikijifua kwenye viwanja vya Gykhana jijini Dar es salaam.

Yanga iliweka kambi ya siku 10 visiwani Zanzibar wakati wa mapumziko ya kalenda ya FIFA, ilikuwa kambi ya kimkakati sehemu ya maandalizi ya mchezo huo wa kwanza kundi B.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wanakwenda Zanzibar huku wakiwa na matarajio makubwa ya kufanya vyema siku ya Jumamosi.

Kamwe amesema kauli mbiu ya Yanga kuelekea hatua ya makundi ni KUBONDA kila atakayeshuka dimba la New Amaan Complex na kwenda KUNYONGA ugenini.

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 24 2026
2h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
Maandalizi ya kuikabili MC Alger yanaendelea Gymkhana
16h ago
READ MORE β†’
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
MC Alger wamfuta kazi kocha kuelekea mchezo dhidi ya Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
Kazimoto amkosha Juma Abdul, ampa somo
18h ago
READ MORE β†’
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
Wanahabari wajitokeza Yanga Media Day
18h ago
READ MORE β†’
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
Injinia Hersi atabiriwa makubwa CAF
1d ago
READ MORE β†’
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
1d ago
READ MORE β†’
Dube aipa ubingwa wa kihistoria Hardrock FC
Dube aipa ubingwa wa kihistoria Hardrock FC
2d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
2d ago
READ MORE β†’