Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22m ago
Yanga vs MC Alger, mechi ya kisasi Jumamosi, CAFCL

Mikiki mikiki ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) inaanza kutimua vumbi mwishoni mwa wiki hii, huku mabingwa wa Tanzania, Yanga, wakijiandaa kuikaribisha MC Alger ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa Kundi B.

Mtanange huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali utapigwa Jumamosi, Novemba 28, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar, huku Wananchi wakiwa na kumbukumbu chungu dhidi ya wapinzani hao.

Kwa mashabiki wa Yanga, huu si mchezo wa kawaida, bali ni mtanange wa kisasi baada ya MC Alger kuwanyima nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo misimu miwili iliyopita.

Katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Yanga ilihitaji ushindi pekee ili kujihakikishia tiketi ya robo fainali, lakini ndoto hizo zilizimwa baada ya kulazimishwa sare tasa ya 0-0.

Matokeo hayo yaliwaacha Wananchi na maumivu makubwa, hasa ikizingatiwa kwamba katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa nchini Algeria, Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-0.

Safari hii, upepo unaweza kuvuma tofauti. Yanga inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na nafasi ya kulipa kisasi mbele ya mashabiki wake na, muhimu zaidi, kuanza kampeni ya hatua ya makundi kwa ushindi.

Ushindi dhidi ya MC Alger hautakuwa tu mwanzo mzuri kwa Wananchi, bali pia utakuwa ujumbe mzito kwa wapinzani wengine wa Kundi B kwamba Yanga imeingia kwenye michuano hiyo ikiwa na malengo makubwa.

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Novemba 23 2026
1h ago
READ MORE β†’
Dube aipa ubingwa wa kihistoria Hardrock FC
Dube aipa ubingwa wa kihistoria Hardrock FC
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Novemba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar kutoka Moshi
Yanga yarejea Dar kutoka Moshi
1d ago
READ MORE β†’
Shalulile mabao saba Ligi Kuu, bado kuna maswali?
Shalulile mabao saba Ligi Kuu, bado kuna maswali?
1d ago
READ MORE β†’
Mzize huyo anarudi kwenye makali yake
Mzize huyo anarudi kwenye makali yake
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Highlights; Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
2d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 21 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 21 2026
2d ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
2d ago
READ MORE β†’
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
2d ago
READ MORE β†’