Kikosi cha Yanga kimewasili mkoani Kilimanjaro kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania.
Mchezo huo utapigwa kesho Ijumaa, Novemba 20 katika uwanja wa Ushirika.
Yanga ilikamilisha maandalizi yake ya mwisho jijini Dar es salaam kabla kukwea pipa kuelekea Moshi majira ya jioni.
Wananchi wamewasili Moshi wakiwa na dhamira moja tu, kuondoka na alama tatu muhimu ugenini.