Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1d ago
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania

Kocha wa mipira ya kutenga wa Yanga, Kagisho Dikgacoi, amesema kikosi hicho kipo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa kesho Ijumaa, Novemba 20, 2026, kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi, mkoani Kilimanjaro.

Dikgacoi amesema maandalizi yaliyofanywa na kikosi hicho kupitia kambi ya Zanzibar yamekuwa na manufaa makubwa, hasa katika kuwajengea wachezaji uelewa wa mfumo na mbinu za kocha mpya.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, utakaopigwa kuanzia saa 10:00 jioni, kocha huyo ameeleza kufurahishwa na mwitikio wa wachezaji katika kupokea maelekezo ya benchi la ufundi.

“Tunaamini timu ipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Polisi Tanzania. Tulifanya maandalizi mazuri kupitia kambi yetu ya Zanzibar, ambapo wachezaji wameonesha mwitikio mzuri kwa kocha mpya na mbinu mpya za kiufundi tunazoanza kuzifanyia kazi,” amesema Dikgacoi.

Kocha huyo ameongeza kuwa wachezaji wameonyesha utayari wa kujifunza na kuendana na mfumo mpya, jambo linaloongeza matumaini kuelekea mchezo huo.

Aidha, Dikgacoi amesema wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya kuzitumikia timu zao za taifa wameanza kuungana na wenzao kikosini tangu jana Jumatano.

“Wachezaji wameonesha utayari wa kujifunza na kuendana na mfumo mpya. Pia, wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya timu zao za taifa wameungana na kikosi kuanzia jana. Tunatarajia kufanya mazoezi mengine mazuri leo ili kukamilisha maandalizi yetu kuelekea mchezo wa kesho,” ameongeza.

Yanga itashuka dimbani kesho ikiwa na dhamira ya kusaka pointi tatu muhimu dhidi ya Polisi Tanzania, katika mchezo utakaokuwa sehemu ya ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu ya NBC baada ya mapumziko ya kupisha michezo ya kimataifa ya timu za taifa (FIFA Break).

Macho ya mashabiki wa Wananchi yatakuwa kwenye namna kikosi hicho kitakavyoonyesha mbinu mpya za kiufundi za kocha Fadlu Davids baada ya maandalizi yaliyofanyika Zanzibar.

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
13h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Happy Birthday GSM
Happy Birthday GSM
1d ago
READ MORE β†’