Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuelekea mkoani Kilimanjaro leo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo Ali Kamwe amesema beki Ibrahim Bacca hatakuwa sehemu ya mchezo huo.
Kamwe amesema Bacca ambaye alipata majeraha wakati anaitumikia timu ya Taifa, anatarajiwa kufanyiwa vipimo zaidi kubaini ukubwa wa majeraha hayo.
Licha ya kucheza mechi zote mbili za Stars dhidi ya Nigeria, Bacca alionekana kutokuwa katika utimamu wa asilimia 100.
Aidha Kamwe amesema ukiondoa Bacca wachezaji wengine ambao walikuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa watakuwa tayari kwa mchezo dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa kesho Ijumaa uwanja wa Ushirika.