Dladla atimka Yanga, kutua Richards Bay Afrika Kusini

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1d ago
Dladla atimka Yanga, kutua Richards Bay Afrika Kusini

Kocha msaidizi wa Yanga SC, Simo Dladla, ameachana na mabingwa hao wa Tanzania Bara na anatarajiwa kurejea nchini Afrika Kusini kuinoa klabu ya Richards Bay FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Betway Premiership.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na mtandao wa FARPost wa Afrika Kusini, Dladla na Yanga wamefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wao, huku kocha huyo akiwa tayari amekubaliana na Richards Bay kuhusu kuiongoza timu hiyo.

Dladla alijiunga na Yanga Julai mwaka huu akiwa msaidizi wa kwanza wa Manqoba Mngqithi, ambaye baadaye aliondolewa katika nafasi ya ukocha mkuu kufuatia sare ya bila kufungana dhidi ya TRA United.

Baada ya kuondoka kwa Mngqithi, Dladla alikabidhiwa jukumu la kuinoa Yanga kwa muda, akifanikiwa kushinda michezo yote miwili aliyosimamia katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Katika mchezo wake wa kwanza, Oktoba 27, aliiongoza Yanga kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Mashujaa FC kabla ya kuichapa Kagera Sugar mabao 4-0, Novemba 1.

Mabadiliko benchi la ufundi Yanga

Awali, Dladla alitarajiwa kuendelea kuwa sehemu ya benchi la ufundi la Yanga chini ya kocha mkuu mpya, Fadlu Davids, lakini sasa ameamua kurejea nchini kwao.

Kuondoka kwake kunaendeleza mabadiliko katika benchi la ufundi la Wananchi kufuatia ujio wa Davids, ambaye ameongeza makocha wasaidizi Darian Wilken na ndugu yake, Maahier Davids.

Dladla anaungana na Tshepang Mokaila na Thulani Thekiso, ambao pia walikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Mngqithi kabla ya kuondoka Yanga.

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
13h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’