Kiungo mshambuliaji wa Yanga Albert Kangwanda ambaye yuko kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ya Zambia, amejumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoikabili Burundi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2027.
Kangwanda alipata majeraha kwenye mchezo uliopita akitolewa uwanjani kwa machela na kuibua hofu kwa mashabiki wa Yanga ambao timu yao imekumbwa na mfululizo wa majeraha kwa mastaa wake.
Hata hivyo kitendo cha kocha George Lwandamina kumjumuisha kwenye kikosi kinachoikabili Burundi leo huku akianza kwenye kikosi cha kwanza ni wazi kuwa nyota huyo yuko fit kwa asilimia 100.
Kangwanda anatarajiwa kurejea nchini mara baada ya mchezo huo kuwahi mtanange wa ligi kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaopigwa Ijumaa Novemba 20 uwanja wa Ushirika, Moshi.