Baada ya sita za mazoezi kisiwani Zanzibar, kikosi cha Yanga leo kilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya KVZ.
Matokeo ya mchezo huo yamewashuhudia Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1 katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa Maisara, Unguja
Mshambuliaji Ibrahima Toure alikuwa shujaa wa Yanga kwenye mchezo huo akipachika mabao mawili huku bao la tatu likifungwa na Edmund John.
Huo ulikuwa mchezo wa kwanza wa kirafiki kwa kocha Fadlu Davids tangu akabidhiwe mikoba ya kuinoa Yanga.