Wakati Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) jana likitangaza orodha ya wachezaji wanaowania tuzo mbalimbali msimu wa 2025/26, kiungo kiraka wa Yanga Duke Abuya hajatajwa katika tuzo zozote.
Ukizungumzia wachezaji waliokuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Yanga msimu uliopita, Abuya ni mmoja wa wachezaji hao.
Anaweza asiwe na takwimu nzuri sana za kufunga na kutoa asisti kutokana na nafasi anayocheza lakini hilo haliondoi mchango wake mkubwa aliotoa msimu uliopita.
Eneo la kiungo bora wachezaji waliotajwa kuwania tuzo hiyo ni Allan Okello, Maxi Nzengeli na Pacome Zouzoua kutoka Yanga, Feisal Salum wa Azam Fc na Clatous Chama wa Simba.
Aidha wanaowania tuzo ya MVP ni nyota hao wote wanaowania tuzo ya kiungo bora wakiongezeka Ibrahim Bacca (Yanga), Ndumumwe Mosi (Singida BS) na Rushine de Reuck (Simba).
Abuya angeweza kuingia kwenye kinyang'anyiro katika tuzo hizo mbili