Kamwe amaliza utata kuhusu mkataba wa Pacome na Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Nov 2026
Kamwe amaliza utata kuhusu mkataba wa Pacome na Yanga

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga, Ali Kamwe, amezungumzia hatma ya kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Pacome Zouzoua, na kuweka wazi msimamo wa klabu kuhusu mkataba wake, huku akifichua kuwa nyota huyo bado anaendelea kuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi licha ya kuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Kupitia taarifa yake, Kamwe amesema Pacome amesafiri alfajiri ya leo kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kuendelea na matibabu, hatua ya tatu (Phase ya 3), ambapo atakaa nchini humo kwa kipindi cha wiki nne ili kupata matibabu zaidi.

Ameeleza kuwa gharama zote za matibabu hayo zinalipwa na uongozi wa Yanga chini ya Rais wa klabu hiyo, Eng. Hersi Said, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha mchezaji huyo anapata huduma bora za kitabibu na kurejea katika hali yake nzuri.

Katika hatua nyingine, Kamwe amemaliza utata kuhusu mkataba wa Pacome na Yanga, akibainisha kuwa mchezaji huyo bado anaendelea kutumikia mkataba wake na klabu hiyo na analipwa stahiki zake zote kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo.

Stahiki hizo zinajumuisha mshahara pamoja na bonasi mbalimbali za ushindi ambazo timu imekuwa ikizipata, jambo linaloonesha kuwa licha ya kutokuwa uwanjani kwa sasa, Pacome bado anatambuliwa kama sehemu ya familia ya Yanga.

Kamwe pia amekumbusha namna ambavyo uongozi wa Yanga umekuwa ukisimamia matibabu ya wachezaji wake wanapokumbwa na majeraha, akitolea mfano wa Dickson Job na Clement Mzize ambao nao walikamilisha hatua zao za mwisho za matibabu nchini Afrika Kusini baada ya kufanyiwa upasuaji wa majeraha ya goti.

Aidha, amewataja wachezaji wengine ambao waliwahi kusafirishwa kwenda Tunisia kwa ajili ya matibabu mbalimbali kuwa ni Yao Yao, Aboutwaleeb Mshery na Shomari Kibwana.

Yanga SC Stories

Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
Goals : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
FT : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, NBC PL
10h ago
READ MORE β†’
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Kikosi : JKT Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
13h ago
READ MORE β†’
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Mudathir amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
18h ago
READ MORE β†’
Dladla awaaga Wananchi
Dladla awaaga Wananchi
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
Matchday; Polisi Tanzania vs Yanga, NBC PL, Nov 20
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 20 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
Yanga yawasili Moshi tayari kuikabili Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
Yanga yakamilisha maandalizi tayari kuifuata Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
Dikgacoi atamba Yanga ipo tayari kuivaa Polisi Tanzania
1d ago
READ MORE β†’