Pacome asafiri Ufaransa kukamilisha awamu ya mwisho ya matibabu yake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28m ago
Pacome asafiri Ufaransa kukamilisha awamu ya mwisho ya matibabu yake

Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Yanga SC, Pacome Zouzoua, ameelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya kukamilisha awamu ya mwisho ya matibabu yake kabla ya kurejea rasmi katika uwanja wa kucheza soka.

Pacome amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi mitano kutokana na jeraha alilopata kwenye mchezo wa ligi kuu mwishoni mwa msimu uliopita dhidi ya JKT Tanzana. 

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Pacome ameeleza kuwa safari ya kupona inaendelea, huku akithibitisha kuwa ameelekea Ufaransa kuanza hatua ya mwisho ya matibabu na kurejesha makali yake ya kimchezo.

Aidha, amekiri kuwa kipindi cha kuuguza jeraha hakikuwa rahisi, lakini kimemfundisha kuwa mvumilivu, mwenye uvumilivu wa changamoto na kutokata tamaa katika mazingira yoyote.

Sambamba na hilo, Pacome amewashukuru mashabiki wa Yanga, maarufu kama Wananchi, pamoja na watu wote ambao wamekuwa pamoja naye, wakimpa moyo na kumuunga mkono katika kipindi chote ambacho amekuwa akipambana kurejea dimbani.

Nyota huyo ameonesha matumaini makubwa kwamba sehemu ngumu zaidi ya safari yake ya kupona huenda imepita, na kwa sasa anahitaji kuelekeza nguvu zake katika matibabu na mazoezi ya kurejesha utimamu wa mwili.

Hatua hiyo inaleta matumaini kwa mashabiki wa Yanga wanaosubiri kwa hamu kurejea kwa kiungo huyo mshambuliaji ambaye amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha timu hiyo.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maxi abaki Dar, sababu yatajwa
Maxi abaki Dar, sababu yatajwa
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 11 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 11 2026
1h ago
READ MORE β†’
Job afunguka kambi ya Yanga Zanzibar
Job afunguka kambi ya Yanga Zanzibar
13h ago
READ MORE β†’
Fadlu anataka boli litembee Yanga
Fadlu anataka boli litembee Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Edna Lema aibukia Mashujaa Queens
Edna Lema aibukia Mashujaa Queens
18h ago
READ MORE β†’
Okello kurejea Yanga?
Okello kurejea Yanga?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 10 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 10 2026
1d ago
READ MORE β†’
Siku ya pili ya maandalizi Zanzibar
Siku ya pili ya maandalizi Zanzibar
1d ago
READ MORE β†’
Job, Mzize wabaki Stars ikisafiri Nigeria
Job, Mzize wabaki Stars ikisafiri Nigeria
1d ago
READ MORE β†’
Kila mmoja atapambania nafasi yake uwanja wa mazoezi
Kila mmoja atapambania nafasi yake uwanja wa mazoezi
1d ago
READ MORE β†’