Klabu ya Wanawake ya Mashujaa Queens imemuajiri aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga Princess Edna Lema.
Lema ameibukia kwa kinadada hao wa mkoani Kigoma baada ya kuondoka Yanga Princess.
Uamuzi wa Yanga Princess kuachana na Edna ulifikiwa baada ya kipigo dhidi ya Simba Queens kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii mwezi uliopita.
Wakati Edna akitimkia Kigoma, Yanga Princess ikinolewa kwa muda na Said Maulid 'SMG', imeanza vyema msimu wa ligi kuu ya Wanawake 2026/27 ikishinda mechi zote mbili za mwanzo huku wakipachika mabao matano.
ADVERTISE HERE