Kocha Mpya wa Yanga Fadlu Davids ametua na wataalamu wawili watakaoimarisha benchi lake la ufundi.
Aliotua nao leo ni Darian Wilken ambaye anakuwa Kocha Msaidizi wakati Parfomance & Video Analyst akiwa ni Mueez Kajee.
Wataalam hao wote walikuwa sehemu ya benchi la ufundi la Fadlu wakati wote wakiwa klabu ya Simba na baadae Raja Casablanca ya Morocco.
Aidha, anga tayari imeachana na mmoja wa wachambuzi wa video (Video analyst), Thulani Thekiso baada ya kuitumikia klabu hiyo kwa miaka minne.
Huenda baadhi ya wataalam waliokuwa kwenye benchi la ufundi la kocha Manqoba Mngqithi wakaendelea na majukumu yao.
Jumapili Yanga inaelekea visiwani Zanzibar kuweka kambi ya siku 10 ambapo benchi jipya la ufundi likawekwa hadharani.
ADVERTISE HERE