Nimefurahi kujiunga na Yanga - Fadlu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
46m ago
Nimefurahi kujiunga na Yanga - Fadlu

Kocha Mkuu wa Yanga Fadlu Davids ameeleza furaha yake baada ya kurejea nchini kwa mara ya pili sasa akijiunga na mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.

Akizungumza muda mfupi baada ya kutua JNIA, Fadlu amesema kujiunga na Yanga ni jambo kubwa kwake na yuko tayari kwa majukumu aliyopewa.

"Najisikia faraja, Tanzania ni kama nyumbani, watu wa nchi hii ni wakarimu na wana upendo. Nimefurahi kurudi tena na zaidi kujiunga na klabu hii kubwa"

"Nilipokea simu kutoka kwa Rais wa klabu na kunieleza kuhusu 'project' iliyopo, Yanga imekuwa na mafanikio makubwa katika misimu mitano na sasa tunataka kujijenga upya ili kuendeleza nmafanikio hayo"

"Tutaboresha staili yetu ya uchezaji, kuifanya Yanga kuwa bora zaidi ili kuendeleza mafanikio tuliyonayo. Sio mara ya kwanza mimi kupokea simu ya Rais (injinia Hersi), hii ni mara ya tatu nafikiri lilikuwa ni suala la muda, kila jambo linatokea katika wakati wake sahihi"

"Sasa niko hapa tayari kwa majukumu makubwa yaliyo mbele, najua msimu haujawa mzuri sana mpaka sasa lakini tuna ligi ya mabingwa mbele yetu. Mimi ni kocha mshindani niko tayari kushindana"

"Wanasema Yanga iko kwenye kundi la kifo lakini hakuna jambo lisilowezekana. Yanga ina wachezaji wazuri sana, ukiangalia timu nzima kila eneo kuna ubora"

"Tutafanya kazi hatua kwa hatua kwenye uwanja wa mazoezi kujenga mfumo wetu wa uchezaji ambao utatufanya tujivunie na kurejesha furaha ya mashabiki wetu na hatutapumzika mpaka turudi kwenye nafasi yetu juu," alisema Fadlu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kazi ndio inaanza, Fadlu ni rasmi
Kazi ndio inaanza, Fadlu ni rasmi
1h ago
READ MORE β†’
Fadlu alivyotua, ujumbe wake kwa Wananchi
Fadlu alivyotua, ujumbe wake kwa Wananchi
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Novemba 07 2026
1h ago
READ MORE β†’
Yanga kuweka kambi ya muda mfupi Zanzibar
Yanga kuweka kambi ya muda mfupi Zanzibar
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya yanaendelea KMC Complex
Maandalizi ya yanaendelea KMC Complex
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki ameanza kwa kusuasua lakini namba zinaongea
Aziz Ki ameanza kwa kusuasua lakini namba zinaongea
19h ago
READ MORE β†’
Nini matarajio Fadlu kutua Yanga?
Nini matarajio Fadlu kutua Yanga?
21h ago
READ MORE β†’
Maxi na msimu wa maajabu Yanga
Maxi na msimu wa maajabu Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
1d ago
READ MORE β†’
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
1d ago
READ MORE β†’