Maxi na msimu wa maajabu Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Maxi na msimu wa maajabu Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Maxi Mpia Nzengeli, anaendelea kuandika historia yake katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania msimu wa 2026/2027, akionyesha kiwango cha juu kinachomfanya kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotikisa soka la Tanzania kwa sasa.

Maxi si tu kwamba amekuwa mhimili muhimu katika kikosi cha Yanga, bali pia amejijengea heshima kutokana na uwezo wake wa kuathiri mwenendo wa mchezo. Katika mechi 10 alizocheza, nyota huyo ameibuka mchezaji bora wa mechi (Man of the Match) mara sita, rekodi inayomfanya kuwa kinara wa tuzo hiyo kwa sasa.

Idadi hiyo inamuweka mbele ya wachezaji wengi wenye majina makubwa, akiwemo winga wa Simba, Libasse Gueye, ambaye ameshinda tuzo hiyo mara tatu.

Ukiangalia mchango wake ndani ya uwanja, unaona wazi kwa nini Maxi amekuwa mchezaji wa thamani kubwa kwa Wananchi. Katika mechi 10 za Yanga kwenye ligi msimu huu, amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mwisho zilizozaa mabao.

Hiyo ina maana amehusika moja kwa moja katika mabao sita kati ya 23 yaliyofungwa na Yanga, sawa na mchango wa karibu asilimia 26 ya mabao yote ya timu hiyo.

Uwezo wake wa kucheza maeneo tofauti uwanjani umemfanya kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Wananchi msimu huu. Pengine ndiye mchezaji aliyecheza dakika nyingi zaidi kwenye kikosi cha Wananchi akichuana na beki Ibrahim Bacca.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Novemba 06 2026
2h ago
READ MORE β†’
Abuya, Yao warejea mazoezini baada ya kupona majeraha
Abuya, Yao warejea mazoezini baada ya kupona majeraha
12h ago
READ MORE β†’
Mpango wa kumshusha Ramovic umekwama, Yanga yarudi kwa Fadlu
Mpango wa kumshusha Ramovic umekwama, Yanga yarudi kwa Fadlu
17h ago
READ MORE β†’
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga
Dladla amejihakikishia nafasi yake Yanga
22h ago
READ MORE β†’
Happy Birthday Mwamnyeto
Happy Birthday Mwamnyeto
22h ago
READ MORE β†’
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
Novemba 5 itaendelea kukumbukwa na Wananchi
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
Magazeti ya leo Alhamisi Novemba 05 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga Princess yaandikisha ushindi wa pili ugenini WPL
Yanga Princess yaandikisha ushindi wa pili ugenini WPL
1d ago
READ MORE β†’
Alama tisa nyumbani CAFCL ni lazima
Alama tisa nyumbani CAFCL ni lazima
1d ago
READ MORE β†’
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
1d ago
READ MORE β†’