Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Adnan Behlulovic humwambii kitu kwa Yanga

Kocha wa viungo Adnan Behlulovic ameendelea kutoa ishara zinazozua maswali kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku tetesi za kurejea kwake Jangwani zikiwa bado zinavuma.

Kwa takribani wiki moja sasa, jina la Adnan limekuwa likitajwa kuhitajika na Wananchi baada ya kusitishwa mkataba wa Chyna Mokayla aliyekuwa kocha wa viungo.

Kocha huyo amekuwa akitumia kurasa zake za mitandao ya kijamii kuweka picha za kumbukumbu za matukio mbalimbali aliyoyafanya akiwa na Yanga, jambo linalozidi kuchochea hisia za mashabiki kuhusu uwezekano wa kurejea kwake.

Kwa sasa, Yanga inatajwa kuwa katika mipango ya kumrejesha kocha Sead Ramovic, ambaye aliwahi kuinoa timu hiyo katika awamu ya kwanza. Ikumbukwe kuwa Adnan Behlulovic alikuwa sehemu ya benchi lake la ufundi wakati huo.

Endapo mpango wa kurejea kwa Ramovic utafanikiwa, uwezekano wa Adnan kurejea Jangwani kwa mara ya pili unaweza kuwa mkubwa zaidi. Hata hivyo, mpaka sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka kwa klabu kuhusu kurejea kwa kocha huyo.

HISTORIA YA ADNAN BEHLULOVIC NDANI YA YANGA

Adnan Behlulovic alijiunga rasmi na Yanga SC Novemba 15, 2024, akiletwa na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Sead Ramovic.

Akiwa ndani ya kikosi cha Wananchi, Adnan alihusika zaidi na maandalizi ya viungo na utimamu wa miili ya wachezaji. Pia alitajwa kuwa na mchango katika kuwasaidia wachezaji kurejea kwenye hali nzuri ya ushindani baada ya kukabiliwa na majeraha.

Hata hivyo, safari yake ndani ya Yanga haikuwa ndefu kwani aliondoka Februari 4, 2025, kufuatia kuondoka kwa Sead Ramovic.

BAADA YA KUONDOKA YANGA

Baada ya kuondoka Jangwani, Adnan amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kujiunga na Azam FC. Aidha, ameendelea kujihusisha na shughuli za ukocha wa vijana, ikiwemo timu ya U19 ya FK Zeljeznicar Sarajevo.

YANGA BADO KIMYA KUHUSU KOCHA MPYA

Wakati huohuo, Yanga bado haijamtangaza rasmi kocha wake mkuu mpya, licha ya uongozi wa klabu hiyo kueleza kuwa kocha anayetarajiwa tayari yupo nchini na kwamba atatangazwa wakati wowote.

Hali hiyo imeendelea kuongeza hamasa na maswali miongoni mwa mashabiki wa Yanga, ambao wanasubiri kuona sura zitakazoongoza benchi la ufundi katika kipindi kijacho.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
Ratiba ya mwisho wa mwaka usipime
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Novemba 04 2026
5h ago
READ MORE β†’
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
Kazini kwa Kibwana bado kuna kazi
17h ago
READ MORE β†’
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
Shalulile atabiriwa makubwa msimu huu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
Yanga kurudi New Amaan Complex makundi CAFCL?
1d ago
READ MORE β†’
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
Nyota tisa wa Yanga kwenye majukumu ya timu za Taifa
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Novemba 03 2026
1d ago
READ MORE β†’
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
Pacome aongeza matumaini ya kurejea mapema
1d ago
READ MORE β†’
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
Kwa Toure hapa Yanga imepata mshambuliaji
2d ago
READ MORE β†’
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
Kangwanda ana kazi ya kufanya Yanga
2d ago
READ MORE β†’