Dladla atabiri mechi ngumu dhidi ya Kagera Sugar, ataka Wananchi kujitokeza kwa wingi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4h ago
Dladla atabiri mechi ngumu dhidi ya Kagera Sugar, ataka Wananchi kujitokeza kwa wingi

Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga SC, Simon Dladla, ametabiri mchezo mgumu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kesho Jumapili katika dimba la KMC Complex, akisema wapinzani wao wanahitaji matokeo muhimu katika harakati za kujinusuru na kushuka daraja.

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Dladla amesema Yanga inatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Kagera Sugar, kutokana na hali ya timu hiyo kwenye msimamo wa ligi, hivyo wachezaji wanapaswa kujiandaa kikamilifu kwa mchezo huo.

"Tunatarajia mchezo mgumu kesho kwa sababu tunakutana na timu inayopambana kujinasua kwenye hatari ya kushuka daraja. Hivyo, tunategemea kupata upinzani mkubwa, kama ule tuliokutana nao dhidi ya TRA," amesema Dladla.

Amesisitiza kuwa licha ya changamoto inayotarajiwa, Yanga ina malengo makubwa katika mbio za ubingwa na haitaki kupoteza alama katika michezo iliyosalia ya ligi.

Dladla amesema dhamira ya kikosi chake ni kuhakikisha kinamaliza msimu kikiwa katika nafasi ya kwanza, huku kikifanya kila kinachowezekana kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kwa kushinda michezo yote iliyobaki.

"Yanga ni timu kubwa yenye malengo makubwa, na lengo letu kuu ni kumaliza ligi tukiwa nafasi ya kwanza. Tutapambana kwa kila hali kuhakikisha tunarejea kileleni kwa kushinda kila mchezo ulio mbele yetu," ameongeza.

Katika hatua nyingine, Dladla amewataka mashabiki wa Yanga, maarufu kama Wananchi, kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuwapa wachezaji hamasa na sapoti wanayohitaji wanapokuwa uwanjani.

Amesema benchi la ufundi linaendelea kufanya kazi kila siku kuboresha kiwango cha timu na kurekebisha mapungufu yanayojitokeza, lakini amesisitiza kuwa mchango wa mashabiki ni sehemu muhimu ya mafanikio ya kikosi.

"Rai yangu kwa mashabiki wa Yanga ni kujitokeza kwa wingi uwanjani kuipa timu hamasa na sapoti wanayohitaji wachezaji wetu. Tunaendelea kufanya kazi kila siku kuboresha timu na kurekebisha mapungufu yanayojitokeza," amesema.

Ameongeza kuwa uwepo wa mashabiki wengi uwanjani huwapa wachezaji morali na motisha zaidi ya kupambana, akiamini sapoti yao inaweza kuwa chachu muhimu katika kuisukuma timu kupata matokeo mazuri.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize arejeshwa kikosi cha Stars
Mzize arejeshwa kikosi cha Stars
2h ago
READ MORE β†’
Zimbwe Jr atuma ujumbe mzito Kagera Sugar, asema Yanga haijaridhishwa na nafasi ilipo
Zimbwe Jr atuma ujumbe mzito Kagera Sugar, asema Yanga haijaridhishwa na nafasi ilipo
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 31 2026
10h ago
READ MORE β†’
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
Yanga vs Kagera Sugar ni Jumapili hii, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
Nini matarajio urejeo wa pili wa Ramovic?
1d ago
READ MORE β†’
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
Kapteni Beka mbioni kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
Kituo kinachofuata ni Kagera Sugar
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1d ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1d ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2d ago
READ MORE β†’