Wakati kikosi cha Yanga kikitarajiwa kuanza mazoezi ya pamoja keshokutwa Jumatatu, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo Juma Mahadhi amekuwa akijifua kwa nguvu muda wote ambao wachezaji walipewa mapumziko.
Mahadhi aliyetua Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Coastal Union, ni mmoja wa viungo washambuliaji mahiri wanaotabiriwa kuja kufanya mambo makubwa kama 'wataheshimu' vipaji vyao.
Msimu uliopita haukuwa mzuri sana kwake kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali za ndani na nje ya uwanja.
Lakini mwenyewe ameahidi kurejea akiwa imara mara dufu msimu ujao.
"Ninafanya mazoezi asubuhi na jioni kujiweka fiti. Ninaamini ni juhudi na bidii zitakazoniwezesha kutimiza ndoto zangu."

ADVERTISE HERE