Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema mlinzi wa kulia Yao Kouassi ataendelea kukosekana leo kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc kutokana na changamoto ya majeraha inayomkabili.
Kamwe amesema Yao anahitaji wiki moja zaidi kuimarika kabla ya kurejea kikosini kuendelea na majukumu.
Hata hivyo habari njema kwa Wananchi ni kuwa mlinda lango Djigui Diarra sasa amerejea kikamilifu na tayari kuendelea na majukumu yake.
Diarra alipata maumivu ya mgongo yaliyomuweka nje kwa takribani wiki moja.
"Kikosi kiko tayari, kuna changamoto za majeraha ya hapa na pale lakini wachezaji wako tayari ukiondoa Yao Kouassi na Duke Abuya"
"Yao bado hayuko sawa, atahitaji wiki moja zaidi kabla ya kurejea wakati golikipa wetu Diarra ambaye alikosekana kwenye mechi zilizopita, amepona na yuko tayari kuendelea na majukumu yake," alisema Kamwe
Mashabiki wa Yanga leo pia huenda wakamshuhudia Stephane Aziz Ki akirejea kikosini baada ya kumaliza adhabu ya kadi nyekundu wakati Mudathir Yahya yeye akikosekana akianza kutumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopata kwenye mchezo uliopita
Aidha kiungo Fredy Ngoma na winga Albert Kangwanda nao walipata majeraha madogo kwenye mchezo dhidi ya TRA United ambapo uwezekano wa kutumika leo utategemea na hali zao baada ya vipimo vya mwisho vya daktari wa timu
Nyota hao walishiriki mazoezi ya mwisho ya jana kuelekea mtanange wa leo