Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga watashuka uwanja wa KMC Complex kuikabili Mashujaa Fc.
Ni mchezo wa raundi ya 9 Wananchi wakihitaji ushindi ili kurejesha morali yao juu kwenye mapambano ya kutetea taji la ligi kuu kwa msimu wa sita mfululizo.
Yanga haina tena nafasi ya kudondosha alama baada ya kukosa ushindi katika mechi mbili zilizopita kwenye ligi.
Matokeo hayo ya mechi zilizopita yalipelekea kufutwa kazi kwa kocha Manqoba Mngqithi ambapo Kocha Msaidizi Simo Dladla amekabidhiwa mikoba kukiongoza kikosi cha Yanga kwenye mchezo huo.
Dladla amesema leo wanahitaji kushinda mchezo huo akiwataka wachezaji wake kupambana na kujitoa kwa ajili ya kuwapa furaha mashabiki wao.
Amesema Yanga inapaswa kuwa timu namba moja hivyo leo wanahitaji kuonyesha ukubwa wao kwa kushinda mchezo pamoja na kucheza soka la kuvutia.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa saa 12:30 jioni..