Hersi akimpata huyu wamekwisha!

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3h ago
Hersi akimpata huyu wamekwisha!

Mabingwa wa kihistoria wa soka nchini Tanzania, Yanga SC, wanaripotiwa kuingia vitani kuwania saini ya kocha mwenye wasifu mkubwa barani Afrika, Krunoslav Jurcic.

Raia huyo wa Croatia anatajwa kuwa chaguo namba moja la viongozi wa klabu hiyo katika kusaka mafanikio makubwa zaidi ya kimataifa.

Habari za ndani kutoka ndani ya klabu ya Yanga SC zinaeleza kuwa mazungumzo ya chinichini tayari yameanza kati ya bilionea na mdhamini mkuu wa klabu hiyo kupitia kampuni ya GSM, na wawakilishi wa kocha huyo ili kukamilisha dili hilo mapema iwezekanavyo.

Jurcic, ambaye kwa sasa yuko huru baada ya kumaliza mkataba wake na miamba ya soka ya Misri, Pyramids FC, anatambulika kama mmoja wa makocha bora na wenye mikakati thabiti zaidi barani Afrika kwa sasa.

Akiwa na Pyramids, kocha huyo mwenye umri wa miaka 56 aliiwezesha timu hiyo kutwaa mataji matano makubwa ndani ya miaka miwili, ikiwa ni pamoja na ubingwa wa kihistoria wa CAF Champions League msimu wa 2024/25 pamoja na Kombe la CAF Super Cup.

Jurcic anaweza kuwa chaguo sahihi Yanga kwani hata mfumo anaopendelea wa 4-2-3-1 unaendana kwa asilimia mia moja na mfumo ambao Yanga wameutumia kwa miaka mingi kabla ya ujio wa Manqoba Mngqithi ambaye alipendelea kutumia washambuliaji wawili.

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) liliwahi kumtaja Jurcic kama mmoja wa makocha wa soka la kisasa barani hapa. 

Hata hivyo mpaka sasa bado hakuna taarifa juu ya kufikiwa kwa makubaliano yoyote Yanga ikiwa bado inaendelea na mchakato.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
2h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
23h ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumapili, Oct 25 2026
Magazeti ya leo Jumapili, Oct 25 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yametimia, Manqoba afutwa kazi Yanga
Yametimia, Manqoba afutwa kazi Yanga
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba mambo magumu Yanga
Manqoba mambo magumu Yanga
1d ago
READ MORE β†’