Wiliete Sc wameangusha mbuyu ligi ya mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2h ago
Wiliete Sc wameangusha mbuyu ligi ya mabingwa

Mamelodi Sundowns jana walikumbana na matokeo wasiyoyatarajia wakitupwa nje ya michuano ya ligi ya mabingwa (CAFC) baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Wiliete Sc ya Angola.

Wiliete wamefuzu kwa faida ya bao la ugenini baada ya suluhu ya bila kufungana (0-0) kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Angola.

Mashabiki wa Yanga wanaikumbuka Wiliete Sc, walikutana nayo msimu uliopita hatua ya awali na kuiondosha kwa ushindi wa jumla wa mabao 5-0 katika mechi zote mbili.

Lakini msimu huu Wiliete wamejipanga na kufanikiwa kumuondosha bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Matokeo hayo yanawakumbusha mashabiki wa soka kuwa ni lazima kumuheshimu mpinzani wako, timu ndogo huwa ziko kwenye makaratasi tu.

Kipigo hicho cha Sunddowns pia kimewapa tabasamu Wananchi kwani bado hawajasahau kile kilichotokea misimu miwili iliyopita mchezo wa robo fainali dhidi ya Sundowns.

Kama sio bao la Stephane Aziz Ki kukataliwa katika hali ya utata, pengine Yanga ingekuwa tayari imeandika historia ya kucheza nusu fainali ya CAFCL.

Sundowns walinusurika kupitia 'mbeleko ya refa' na wakafanikiwa kuiondosha Yanga kwenye mikwaju ya penati.

Ni wazi msimu huu ipo nafasi kubwa ya Yanga kufanya vyema zaidi kwenye michuano hiyo kwani kwenye makaratasi hakuna timu ya kuihofia baada ya baadhi ya vigogo kukosekana.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; TRA United vs Yanga, NBC PL, Oct 24
Matchday; TRA United vs Yanga, NBC PL, Oct 24
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 24 2026
Magazeti ya leo Jumamosi, Oktoba 24 2026
5h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili TRA United yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili TRA United yamekamilika
16h ago
READ MORE β†’
Manqoba atuma ujumbe kwa wachezaji Yanga 'lazima tupambane kushinda'
Manqoba atuma ujumbe kwa wachezaji Yanga 'lazima tupambane kushinda'
23h ago
READ MORE β†’
Tumejiandaa kushinda dhidi ya TRA United - Masalanga
Tumejiandaa kushinda dhidi ya TRA United - Masalanga
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba akiri TRA United wagumu, aweka mkakati wa kuwadhibiti
Manqoba akiri TRA United wagumu, aweka mkakati wa kuwadhibiti
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yapania alama tatu Arusha
Yanga yapania alama tatu Arusha
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
1d ago
READ MORE β†’
Manqoba tunamuamini - Kamwe
Manqoba tunamuamini - Kamwe
1d ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni TRA United
Kituo kinachofuata ni TRA United
1d ago
READ MORE β†’