Yanga yapania alama tatu Arusha

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Yanga yapania alama tatu Arusha

Kikosi cha Yanga kesho Jumamosi kitashuka uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha kuikabili TRA United katika mchezo wa ligi kuu ya NBC.

Yanga iliwasili Arusha jana tayari kwa mtanange huo ambao Wananchi wanahitaji matokeo ya aina moja tu, ushindi ili kuendelea kusalia katika mapambano dhidi ya watani zao Simba kwenye mbio za ubingwa.

Yanga inashuka dimbani hapo kesho ikitoka kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa baada ya ushindi wa jumla wa mabao 8-1 dhidi ya CFFA ya MAdagascar.

Vijana wa kocha Manqoba Mngqithi wana ari na morali kubwa kuelekea mtanange huo utakaopigwa saa 10 jioni.

Wapinzani wao watamba

Wakati Yanga ikitua Arusha, msemaji wa TRA United Christina Mwagala ametamba kuwa wako tayari kuifunga Yanga kwenye mchezo huo.

Mwagala amedai kuwa kikosi cha Yanga kwa sasa ni dhaifu na hilo linawapa nafasi nzuri ya kushinda mchezo huo.

Kwa upande wa Yanga ni wazi mchezo wanaweza kutumia kuwafunga midomo wale wanaodhani kikosi cha mabingwa hao watetezi ni dhaifu.

Yanga imepoteza mchezo mmoja tu kwenye ligi msimu huu iikikusanya alama 18 baada ya mechi 7 ikishika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 23 2026
4h ago
READ MORE β†’
Manqoba tunamuamini - Kamwe
Manqoba tunamuamini - Kamwe
18h ago
READ MORE β†’
Kituo kinachofuata ni TRA United
Kituo kinachofuata ni TRA United
21h ago
READ MORE β†’
Karibu tena dimbani Job
Karibu tena dimbani Job
23h ago
READ MORE β†’
Yanga kuifuata TRA United leo
Yanga kuifuata TRA United leo
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
Highlights; Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
FT : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
Goals : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Kikosi : Yanga vs CFFA, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’