Karibu tena dimbani Job

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1h ago
Karibu tena dimbani Job

Jana ilikuwa siku ya kipekee kwa mashabiki wa Yanga pale uwanja wa Azam Complex wakiishuhudia timu yao ikiandika rekodi baada ya kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa Afrika kwa msimu wa nne mfululizo.

Ni baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya CFFA ya Madagascar, ushindi ambao uliwahakikishia Wananchi kufuzu makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 8-1.

Lakini pia ilikuwa siku muhimu baada ya kumshuhudia beki na nahodha msaidizi Dickson Job akirejea baada ya muda mrefu wa majeraha.

Job aliingia kwenye kipindi cha pili akichukua nafasi ya nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto.

Mashabiki wa Yanga walisubiri kwa hamu kubwa kumshuhudia Job akirejea tena baada ya kukosakana uwanjani tangu March mwaka huu alipoumia kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex visiwani Zanzibar.

Urejeo wa Job unamaanisha kuimarika zaidi kwa safu ya ulinzi ya Yanga ambayo msimu huu imeshuhudia mabadiliko ya mara kwa mara kwa walinzi wa kati Komara na Mwamnyeto wakipishana au kucheza sambamba na Ibrahim Bacca ambaye jana kocha Manqoba Mngqithi alimpa mapumziko baada ya kutumika mfululizo.

Job atahitaji mechi kadhaa kabla ya kuwa tayari kwa asilimia 100 lakini matarajio ni kuwa hatachukua muda mrefu kurudi kwenye ubora wake.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yanga kuifuata TRA United leo
Yanga kuifuata TRA United leo
1h ago
READ MORE β†’
Highlights; Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
Highlights; Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 22 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
FT : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Goals : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
Goals : Yanga 4-1 CFFA, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs CFFA, CAFCL R2
Kikosi : Yanga vs CFFA, CAFCL R2
18h ago
READ MORE β†’
Yao aungana na Diarra, Abuya kuikosa CFFA
Yao aungana na Diarra, Abuya kuikosa CFFA
22h ago
READ MORE β†’
Yanga kutangulia makundi CAFCL leo? Droo Oktoba 28
Yanga kutangulia makundi CAFCL leo? Droo Oktoba 28
1d ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs CFFA, CAFCL MD2
Matchday; Yanga vs CFFA, CAFCL MD2
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 21 2026
1d ago
READ MORE β†’