Baada ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya CFFA ya Madagascar hapo jana na kujihakikishia tiketi ya kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika (CAFCL), kikosi cha Yanga hakina muda wa kupoteza kwani wanarejesha nguvu kwenye ligi kuu ya NBC.
Jumamosi Oktoba 24 katika uwanja Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha, Yanga inakabiliwa na mchezo wa kiporo wa ligi kuu dhidi ya TRA United.
Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam jioni ya leo kuelekea Arusha tayari kwa mtanange huo.
Wananchi wanahitaji kushinda ili kupunguza gap la pointi dhidi ya watani zao Simba walio kileleni kwa tofauti ya alama 6.
Jana kwenye mchezo dhidi ya CFFA, mkufunzi wa Yanga Manqoba Mngqithi aliwapa mapumziko baadhi ya nyota wake muhimu wa kikosi cha kwanza ili kuhakikisha kikosi chake kinakuwa imara kuwakabili TRA United katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.