Yanga sio tu inataka kutinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa msimu wa nne mfululizo, lakini pia inataka kutumia mchezo wa mkondo wa pili dhidi ya CFFA kutuma ujumbe Afrika kuwa Wananchi wanautaka ubingwa.
Ndio! Yanga hii hii ambayo baadhi ya wachambuzi wanaona kama 'unga-mwana', kocha wake Manqoba Mngqithi ameweka wazi malengo yake ni kutwaa ubingwa wa Afrika akiamini kikosi chake kinaweza kufikia mafanikio hayo.
Mchezo wa mkondo wa kwanza Yanga ilishinda mabao 4-0, kesho Jumatano, timu hizo zinakutana tena kuhitimisha mchezo wa mkondo wa pili pale dimba la Azam Complex, saa 1 usiku.
Kimahesabu Yanga inahitaji ushindi, sare na hata kupoteza kwa chini ya mabao manne, Wananchi wanatinga makundi.
Lakini kwa maandalizi aliyofanya Manqoba na vijana wake, ni wazi Yanga itashuka kwenye mchezo huo ikiwa na lengo la kutafuta ushindi wa pili.
Katika mchezo wa kwanza Yanga ilipoteza nafasi nyingi, kuelekea mchezo wa kesho, Manqoba ameweka wazi kuwa wamefanya kazi kubwa kwenye uwanja wa mazoezi na matarajio yake n vijana wake kuongeza ufanisi mbele ya lango na kutumia vyema nafasi zao.





