Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi uwanja wa Azam Complex siku ya Jumatano Oktoba 21 kwenye mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kufuzu hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika (CAFCL).
Baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya CFFA kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa Azam Complex Yanga ikiwa ugenini, Jumatano hii Wananchi watakuwa nyumbani.
Kamwe amesema Yanga inakribia kuweka historia kwa kuwa klabu ya kwanza Tanzania kucheza hatua ya makundi CAFCL kwa misimu minne mfululizo.
Ushindi au matokeo yoyote ya sare au kupoteza sio kwa zaidi ya mabao matatu, yatawahakikishia Wananchi kufikia rekodi hiyo kwa klabu za Tanzania.
Aidha baada ya kuwa klabu iliyofunga mabao mengi kwenye mechi za mkondo wa kwanza, Kamwe ametamba kuwa wanakwenda kumaliza mechi ya mkondo wa pili na takwimu nzuri zaidi.
"Yanga ndio klabu pekee iliyoshinda magoli mengi kwenye hatua ya pili, mechi za kwanza Ligi ya Mabingwa Afrika.Tukutane tena Jumatano, Azam Complex kumaliza hii kazi tuweke rekodi ya kuwa timu ya kwanza Tanzania kucheza GROUP STAGE ZA CHAMPIONS LEAGUE MARA 4 Mfululizo".
"Mechi ni saa 1:00 Jioni .. Viingilio ni vile vile tutakata kupitia N CARD," aliandika Kamwe kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii